Jeremiah 17:1-6

Dhambi Ya Yuda Na Adhabu Yake


1 a“Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma,
imeandikwa kwa ncha ya almasi,
kwenye vibao vya mioyo yao
na kwenye pembe za madhabahu zao.

2 bHata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao
na nguzo za Ashera,
Ashera ni mungu mke aliyekuwa anaabudiwa na Wakanaani.

kandokando ya miti iliyotanda
na juu ya vilima virefu.

3 dMlima wangu katika nchi pamoja na utajiri
na hazina zako zote nitazitoa ziwe nyara,
pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia miungu
kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote.

4 eKwa kosa lako mwenyewe utaupoteza
urithi niliokupa.
Nitakufanya mtumwa wa adui zako
katika nchi usiyoijua,
kwa kuwa umeiwasha hasira yangu,
nayo itawaka milele.”

5 fHili ndilo asemalo Bwana: “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu,
ategemeaye mwenye mwili
kwa ajili ya nguvu zake,
ambaye moyo wake
umemwacha Bwana.

6 gAtakuwa kama kichaka cha jangwani;
hataona mafanikio yatakapokuja.
Ataishi katika sehemu zisizo na maji,
katika nchi ya chumvi ambapo
hakuna yeyote aishiye humo.

Copyright information for SwhKC